Ismail (katikati) akiwa na Malkia wa nyuki na Kaseja
Mshambuliaji kinda wa Simba, Rashid Ismail ambaye alihudhuria
mara mbili mazoezi ya Yanga na kuzua gumzo kubwa, ameikana timu hiyo.
Ismail ameendelea kusisitiza alikwenda kuangalia mazoezi
akiwa kama mdau wa soka, lakini akasisitiza hakuwahi kuchezea Yanga B kama
ambavyo imekuwa ikielezwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ismail alisema hakuwahi
kuichezea Yanga na timu yake ya kwanza kubwa ni Simba.
“Nimesikia sana taarifa za mimi kucheza Yanga B, inawezekana
watu wananichanganya na mtu mwingine. Sijawahi kabisa, ingekuwa ni hivyo wala
nisingeficha kwa kuwa si kitu kibaya. Naomba uwaeleze, sikuwahi kucheza Yanga,”
alisema Ismail ambaye ni mtaratibu.
Ismail alikuwa katika kikosi cha Simba kilichoundwa na
wachezaji chipukizi wengi, ambacho kiliiangamiza Coasta Union iliyokuwa
imepania kuichapa Simba.
Kutokea kwake katika mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Bora,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam kumezua gumzo kubwa miongozi mwa wadau wa soka
nchini.
Ismaili alihudhuria mazoezi ya Yanga mara mbili, mara ya
kwanza mashabiki wa Yanga walionekana kupandwa jazba baada ya kumuona, lakini
siku moja baadaye akahudhuria tena na kushuhudia mazoezi hadi mwisho chini ya
Kocha, Ernie Brandts.
0 COMMENTS:
Post a Comment