Upasuaji wa uvimbe wa shavu wa
beki wa Yanga, Ladislaus Mbogo umekwenda vizuri na afya yake inaendelea vizuri
katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Salehjembe imemshudia Mbogo
akiwa katika hospitali hiyo, na leo asubuhi wachezaji wa Yanga, mara baada ya
mazoezi ya asubuhi walikwenda kumtembelea.
Upasuaji wa uvimbe wa Mbogo
aliyejiunga na Yanga akitokea Toto African ulifanyika chini wa daktari wa timu
hiyo, Nassor Matuzya.
Mbogo amesema anajisikia vizuri
baada ya kushituka, jana alizinduka kutoka usingizini saa 11 jioni, baada ya
kufanyiwa upasuaji huo kwa zaidi ya saa tatu.
Wachezaji wa Yanga
walimtembelea na kuzungumza naye huku wakitaniana, lakini walilazimika kuingia
kwa makundi kutokana na wingi wao.
Gazeti la Championi lilikuwa la
kwanza kuandika kuwa Mbogo atafanyiwa upasuaji.
Blog hii pia ilikuwa ya kwanza
kutaarifu kuhusiana na hilo na Mbogo maarufu kama Mnyama sasa atakuwa katika
muonekano tofauti.
Hata hivyo, daktari mmoja
katika hospitali ya Mwananyamala, alisema muonekano wake utabadilika taratibu
kulingana na ngozi inavyosinyaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment