Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) limeondoa utaratibu wa wadau wake kuingia bure kwenye mechi kwa kutumia
tiketi maalum (free pass).
Kutokana na uamuzi
huo hakutakuwa tena na pasi za bure kwa ajili ya kushuhudia mechi zilizo chini
ya usimamizi wa moja kwa moja wa TFF katika viwanja mbalimbali nchini.
Uamuzi huo
umetokana na ukweli kuwa free pass zimekuwa zikipunguza au kuchukua mgawo wote
wa TFF kwenye mechi, na wakati mwingine shirikisho hulazimika kutoa fedha za
ziada kugharamia pasi hizo.
Pasi zote ambazo
imekuwa ikitoa kwa wadau wake hukatwa katika mgawo wa TFF katika mechi husika.
Shirikisho hivi sasa linapata asilimia nne tu ya mapato katika mechi za Ligi
Kuu Bara, ligi ambayo hivi sasa inaendeshwa na Kamati yake ya Ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment