Morad, Nyoni na Aggrey wakiwa na kipa Mwadini |
Uongozi wa klabu ya Azam FC, leo
umetangaza kuwarudisha wachezaji wake waliokuwa wanatuhumiwa kuchukua rushwa.
Azam FC imeeleza kwamba imepata
taarifa kutoka Takukuru kuwa wachezaji
hao wameonekana hawana hatia.
Katika ripoti hiyo iliyotolewa na
katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa, Azam imeeleza kuwarudisha kundini.
Azam FC inatoa taarifa rasmi kuwa Takukuru haijawakuta na hatia ya rushwa wachezaji Deogratius Munish, Erasto Nyoni, Said Hussein Morad na Agrey Morris,” ilieleza sehemu ya ripoti hiyo.
“Hivyo wachezaji hao wanakaribishwa rasmi kurudi
kikosini Azam FC kwa ajili ya kujiunga na mazoezi na wachezaji wenzao.”
Azam iliwatuhumu
wachezaji hao kupokea rushwa katika mechi dhidi ya Simba, hivyo ikaamua
kulifikisha tukio hilo Takukuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment