Kituo cha televisheni cha SuperSport cha
Afrika Kusini kitaonesha moja kwa moja mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom katika
Super Week kati ya Aprili 11 na Mei 18 mwaka huu.
Mechi hizo ni kati Azam na African Lyon
itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja
wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Yanga na Oljoro JKT ambayo sasa
itachezwa Aprili 13 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Azam na Simba itakayochezwa Aprili 14 mwaka
huu badala ya Aprili 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, na mechi kati ya Coastal
Union na JKT Ruvu itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka
huu.
Mechi nyingine ya Super Week itakayochezwa
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga
itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu.
Pia mechi nyingine itakayooneshwa live na
SuperSport ni kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Mei 18 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na mechi za Super Week, mechi kati
ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa ichezwe Aprili 13 mwaka huu sasa
itachezwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment