Kocha mpya wa Sunderland, Paolo Di Canio ameweka kando masuala yanayomsakama kama kuhusishwa na siasa na kuanza kazi yake mara moja.
Muitaliano huyo aliongoza mazoezi ya Sunderland katika hali nzuri huku akiwashangaza wengi kutokana na kufanya kazi siku ya kwanza lakini akionekana kama ni mwenyeji.
Di Canio, ambaye alikuwa anajulikana kwa vituko wakati anacheza, amejibandika jina la 'The Unique One’. Akiwa maoezini alionekana kuwasiliana vizuri na wachezaji wake.
Di Canio amechukua nafasi ya Martin O’neill ambaye alitimuliwa hivi karibuni baada ya kufungwa katika mechi kali dhidi ya Man United bao 1-0 na kuzidi kujiweka katika wakati mgumu kubaki LIgi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment