Mazoezi ya
vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga hayana tofauti na mechi au zaidi. Wachezaji wanatiana
‘njaa’ vilivyo na kila mmoja anaonekana amepania mazoezi kweli.
Katika mazoezi
hayo leo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama, Dar. Wachezaji wa Yanga walikuwa
wakicheza kwa ushindani mkubwa.
Hali hiyo
ilisababisha baadhi yao kuumia karibu kila baada ya dakika 15 kutokana na namna
wanavyocheza kazikazi.
Kocha Mkuu,
Ernie Brandts alisema anafurahishwa na namna mazoezi yanavyoendelea na ndiyo
maana anawapa wachezaji muda mwingine wa kucheza mpira.
Lakini anafurahishwa
zaidi kwa kuwa wachezaji wote wanaonekana wanafanya mazoezi siriaz, kitu
kinachompa picha ni kweli wamepanga kumaliza ligi wakiwa mabingwa.
Hata hivyo,
alisisitiza bado wana tatizo la kupoteza nafasi ambalo anaendelea kulifanyia
kazi pamoja na wachezaji wake.
“Mwisho
tutapata jibu, lakini lazima tufanye mazoezi tena na tena ili kuweka mambo
safi,” alisema Brandts.
Ushindani
wa mazoezi hayo ya Yanga, umesababisha watu wengi wawe wanajitokeza zaidi kwa
kuwa yana burudani ya kutosha na wachezaji wanakuwa bize kama wako katika
mechi.
0 COMMENTS:
Post a Comment