Beki wa
kati wa Man United, Rio Ferdinand ni kati ya mabeki wanaokumbwa na dhoruba ya
umri ingawa soka bado limahitaji.
Rio ambaye
alianza kung’ara akiwa na West Ham kabla ya kujiunga na Leeds United ambako
alianza kuonekana ni mmoja wa mabeki bora duniani.
Ubora wa
Rio ulithibitika baada ya kununuliwa kwa dau kubwa zaidi ambalo hakuna beki wa England
amewahi kununuliwa nao wakati akitua Man United.
Amekuwa beki
kisiki, ingawa umri unamtupa mkono, kikubwa cha kujiuliza ni beki mbabe kuliko
wote duniani?
Hali hiyo
inatokana na tabia ya ‘kihuni’ ya Rio katika mechi mbalimbali ambazo amekuwa
akicheza.
Amekuwa akivizia
na kuwapiga ngumi au makofi washambuliaji anaowakaba katika kipindi anachoamini
mwamuzi hamuoni.
Ukiachana na
hivyo, ndiye amekuwa kiongozi wa vurugu zote zinazotokea wakati wa mechi za Man
United.
Kama kutatokea
kutoelewana kati ya wachezaji, basi lazima Rio atakuwa mmoja wa wahusika.
Rio ambaye
baba yake ni Mwingereza mwenye asili ya Jamaica, alizaliwa katika kitongoji cha
Peckham kilicho katika jiji la London.
Pechkam ni
sehemu maarufu kama ‘Uswahilini’ katika jiji hilo, lakini eneo hilo limekuwa
maarufu Uingereza yote.
Umaarufu wake
si wa mambo mema, kumekuwa na vurugu sana na Polisi wamekuwa wakikimbiza kila
kukicha na vijana wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya, wizi na
ubakaji.
Katika
kitabu cha maisha ya Rio, pia anaelezea namna maisha yalivyokuwa magumu wakati
akiwa mdogo katika eneo hilo.
Baba na
mama yake walitengana na yeye, mdogo wake Antoni na dada yao waliishi pamoja na
mama yao.
Inawezekana
hiyo ikawa ni sehemu ya maisha ya ubabe ya Rio, lakini bado anaonekana kuwa
burudani na tishio kwa mafowadi wengi.
Jiulize,
nani ni beki wa aina yake wakati yeye anaporomoshwa kiwango nja umri?
Asingekuwa muingereza nazani angekuwa anakumbwa na azabu kutoka FA lkn ndio hivyo tena mwache afanye anavyotaka
ReplyDelete