April 9, 2013



Teknolojia ya kutumia vivaa maalum vitakavyokuwa vikifanya kazi ya kubaini kama mpira umeshavuka msitari wa goli itaanza kutumika katika Ligi Kuu England msimu ujao.
 
Horne

Teknolojia hiyo maarufu kama goal-line technology (GLT) huenda ikaanza kutumika England msimu ujao kutokana na kauli ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka England (FA), Alex Horne.

Horne amewaambia waandishi wa BBC leo kuwa wanaona ni kitu kizuri na wameishuhudia ikitumika katika Kombe la Dunia na baadhi ya mechi za ligi hiyo.
 
Hii ilikuwa Kombe la Dunia, kati ya Ujerumani na England ilipata bao kupitia mkwaju wa Lampard, lakini mwamuzi hakuona vizuri..

“Tunaona ni kitu kizuri na kitakuwa na msaada mkubwa, majaribio yake yamekuwa na mafanikio na siku chache tutakutana, ninaamini tutapitisha,” alisema Horne.


Tayari Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetoa kazi kwa kampuni ya Kijerumani iitwayo GoalControl ili kufunga mitambo ya GLT katika viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani.

Pamoja na juhudi za kuipinga teknolojia hiyo, mambo yanaonekana kubadilika katika kipindi hiki na teknolojia hiyo inaonekana itaanza kutumika ingawa katika nchi nyingi za Afrika itakuwa vigumu kutokana na vifaa hivyo kuwa ghali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic