Real Madrid ya Jose Mourinho imejiweka
katika nafasi nzuri ya kusonga hadi hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa
Galatasaray ya Uturuki kwa mabao 3-0.
Mabao ya Madrid yalipachikwa na
Cristian Ronaldo, Karim Benzema na Gonzalo Higuain na kuwaacha wageni waliokuwa
wanaongozwa na Didier Drogba wakitoka patupu.
Madrid walionyesha mchezo wa kujiamini
zaidi na kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa hasa katika kipindi cha pili, wakati
Drogba alionekana kufurukuta katika kipindi cha kwanza, lakini hakuwa na
madhara kwa difensi ya Mourinho iliyoongozwa na Sergio Ramos.
Wiki moja baadaye, Madrid itakuwa ugenini
jijini Istambul kusaka sare au ushindi ili kusonga mbele.
Wakati wenyeji hao watatakiwa kushinda
kuanzia mabao manne ili kupata nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu
fainali.
Mechi nyingine ya usiku huu imepigwa
mjini Malaga na wenyeji wakashindwa kufurukuta dhidi ya Borussia Dortimund.
Mechi hiyo kati ya Malaga na Dortimund
imemalizika kwa sare ‘tasa’, hali inayoilazimisha kila timu kutakiwa kusaka
ushindi katika mechi ya pili mjini Dortimund, Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment