Leo mahakamani...
Mshambuliaji wa Manchester City, Carlos Tevez kufanya kazi za kijamii kwa saa 250 pia kakumbana na adhabu ya kusimamishwa kuendesha gari kwa miezi sita.
Pamoja na adhabu hizo mbili, Tevez amekumbana na dhabu ya tatu ya kupigwa faini ya pauni 1,000 (zaidi ya Sh milioni 2.2).
Tevez alipatikana na hatia katika mahakama ya Macclesfield baada ya kukutwa akiendesha gari huku akiwa katika adhabu ya kusimamishwa kuendeshwa lakini pia hakuwa na bima.
Awali kulikuwa na taarifa, huenda Tevez angekutana na kifungo cha miezi sita jela ambayo ndiyo adhabu kubwa zaidi kwa aliyekamatwa na kosa kama lake.
Tevez, 29, alifika mahakamani hapo akionekana kwua na matumaini ya kuepuka kifungo hicho cha miezi sita kama ambavyo ilikuwa mwisho wa kesi hiyo.
Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ukiongozwa na Kate Marchuk, uliiambia mahakama kuwa kati ya muda wa saa 10 jioni, walipata taarifa kuwa Tevez katika eneo la Mottram Hall Hotel na Golf Club huko Cheshire akiendesha gari jeupe aina ya Range Rover.
Alisema walipewa taarifa na msamaria mwema kuhusiana Tevez kuendesha gari hilo wakati ilikuwa inajulikana alikuwa amefungiwa kufanya hivyo kwa miezi sita kuanzia Januari 16 hadi Mei 25, mwaka huu.
Alisema baada ya maofisa wa Polisi kufika katika eneo hilo walimuona Tevez lakini hata hivyo hakuwa akiendesha Range Rover kama walivyoelezwa badala yake gari aina ya Porsche Cayenne, wakati huo tayari ilikuwa ni saa 11 jioni.
Tevez amekuwa akiingia kwenye misukosuko nje ya soka kutokana
na utukutu wake lakini wakati mwingine imeelezwa amekuwa akisumbuliwa na suala
la kutoelewa Kingereza ambacho hata hivyo amekuwa hataki kujifunza.
0 COMMENTS:
Post a Comment