April 8, 2013




Mashabiki wa Barcelona wameondolewa hofu kwa kiasi fulani baada ya taarifa kuenea kuwa mshambuliaji wao Lionel Messi atakuwa fiti kuivaa PSG katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Maandishi aliyoyaweka Messi katika mtandao mmoja wa kijamii akionyesha kufurahia kurejea kwa beki, Abdidal na ushindi walioupata Barcelona, pia amesisitiza anaamini atakuwa fiti kuivaa PSG kwenye Uwanja wa Cam Nou.


“Nina furaha kubwa kurejea kwa Abi, lakini ushindi pia umekuwa muhimu, nawapongeza wenzangu kwa mabao matano waliyofunga na Barcelona inasonga mbele,” amendika Messhi.

“Kuhusiana na kucheza, bado ninapambana na nina imani nitakuwa fiti kabla ya kuivaa PSG, ninafanya juhudi mambo yaende vizuri.”

Messi alicheza dakika 45 katika mechi iliyopita dhidi ya PSG ikiwa ni baada ya kuumia, hivyo akatolewa na kuanzia hapo alipumzishwa.

Mechi hiyo ya mjini Paris ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2, maana yake kila timu itapambana vilivyo katika mechi hiyo inayofuatia ili isonge hadi nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic