April 9, 2013




Beki wa kati ya Man United, Phil Jones amefananishwa na katuni maarufu kwa jina la Beaker.


Jones ambaye alijitahidi kumzuia Kun Aguero kuifunga United bao la pili bila ya mafanikio, picha yake wakati akiangalia mpira uliopigwa na Muargentina huyo ukiingia wavuni ndiyo iliyozua mjadala.

Kutokana na picha hiyo, baadhi ya mitandao ya Uingereza iliweka picha ikimfananisha Jones na Beaker.

Kufanana kulitokana na namna anavyokuwa anashangilia au kushangaa na mdomo wake unavyokuwa lakini kuhusiana na mtindo wake wa nyewele.

Hata hivyo mitandao hiyo imekuwa ikijihami kwamba haina nia mbaya badala yake inashindwa kukaa kimya kutokana na hali ya kufanana kupindukia kati ya Jones na Beaker.

Angalia picha uone mwenyewe halafu utapata jibu sahihi!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic