April 8, 2013




Kim Kardashian ndiye mwanamke staa anayeaminika kusumbuka sana na hali yake ya ujauzito aliyonayo sasa.


Kim ambaye ni mpenzi wa rapa, Kanye West, juzi alionekana akiingia kanisani na mama yake mzazi Kris Jenner jijini Los Angeles akiwa amevaa gauni kubwa.

Gauni alilokuwa amevaa imekuwa tofauti na mengi aliyokuwa akivaa, hali ambayo wataalamu wa mavazi wa E Televisheniw anaeleza ni kama hali ya kusumbuka, kwamba hajui hasa sahihi ni vazi gani linamfaa kwa wakati huu.




Mwanadada huyo maarufu, siku chache kabla, kuna baadhi ya picha zake zilinaswa akiwa anajikagua tumbo lake sehemu inayoaminika ni chumbani mwake.

Hali hiyo ya kutojiamini avae vazi gani imeelezwa kutokana na watambuzi wa mavazi kumueleza kwamba nguo nyingi hazimpendezi.

Tayari ujauzito wa Kim umefikisha miezi sita na baba mtarajiwa Kanye, imekuwa ni mara chache kuongozana na mwanadada huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic