April 9, 2013




Real Madrid imevuka hadi hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuing’oa Galatasaray ya Uturuki kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi.

Hata hivyo kazi haikuwa lahisi baada ya Madrid ambayo ilionekana itakuwa na kazi lahisi kukumbana na kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa wabishi hao wa Istanbul waliokuwa nyumbani.


Madrid walitangulia kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia Ronaldo, walipoingia kipindi cha pili walionekana kuwa na dharau kama vile wako mazoezini.


Galatasaray wanaojulikana kwa ubishi waliendelea kulisakama lando la Madrid na beki wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Ebue akafunga bao la kwanza kwa shuti saafi.

Wesley Sneider akafunga la pili baada ya kuichambua ngome ya Madrid kabla Didier Drogba au Tembo kufunga la tatu kwa kisigizo.

Beki wake arbeloa alilambwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano. Dakika za mwisho, Madrid walilazimika kujihami kuepuka kufungwa mabao mengi zaidi.


Wakati mechi inaenda ukigongoni, Ronaldo alifunga bao la pili katika dakika ya 90 na kufanya matokeo yawe 3-2.

Katika mechi nyingine, Malaga ilishindwa kufuzu katika dakika nne za mwisho baada ya Wajerumani Borussia Dortmund wakiwa nyumbani kucharuka na kufunga mabao mawili ya harakaharaka ambayo yaliwashangaza Wahispania hao waliokuwa na matumaini ya kufuzu.


Malaga nusura ifuzu lakini mabao ya dakika 90 ya Reus na Santana yalibadili matokeo na Dortimund ikafuzu kwa ushindi wa mabao 3-2, mechi ya kwanza mjini Malaga ilimalizika kwa sare  ya bila kufungana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic