Kipigo cha mabao 4-1 walichokitoa Arsenal kwa Wigan
Athletic maana yake timu hiyo ‘roho ya paka’ imeteremka daraja.
Wigan ambao ni mabingwa wa Kombe la FA wameteremka
daraja baada ya kipigo hicho katika Uwanja wa Emirates jijini London.
Wigan ilikuwa inataka ushindi ili ibaki na Arsenal
ilitaka ushindi ili ipate nafasi ya nne na ikiwezekana kuendelea kugombea
nafasi ya tatu katika mechi moja ya mwisho iliyobaki.
Wigan imekuwa ikipambana karibu kila msimu kuwania
kutoteremka daraja, lakini leo ilikuwa siku mbaya kwao.
Wigan imeungana na Reading na QPR kukamilisha timu
tatu zilizoteremka daraja msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment