Mshambuliaji
wa Barcelona, Lionel Messi amesitisha uamuzi wa kuendelea na matibabu,
televisheni ya Catalan ya Channel 'TV3' imeeleza.
Alitakiwa
kwenda hospitali juzi asubuhi lakini hakufanya hivyo na alitakiwa kuchukuliwa
kipimo cha MRI kwa ajili ya kuendelea na matibabu.
Hospitali hiyo
ya Creu Blanca ndiyo ilikuwa ikimpatia matibabu na imekuwa ikishughulika na
matibabu ya wanamichezo mbalimbali.
Uamuzi wake
wa kugoma kuendelea na matibabu katika hospitali hiyo umewashangaza watu wengi
lakini Messi akashikilia msimamo wake.
Kutokana na
hali hiyo, madaktari wa Barcelona walilazimika kuwasiliana na uongozi ambao
ulifanya mawasiliano na Messi ambaye alishikilia msimamo huo.
Baadaye
walipojadiliana, walikubalia Messi afanyiwe vipimo katika kituo maalum cha
mambo ya afya kinachomilikiwa na Barcelona.
Ingawa uongozi
wa Catalunya haujathibitisha kuhusiana na nilo lakini kweli Messi alifanyiwa
vipimo Sant
Joan DespĂ inayomilikiwa na klabu hiyo.
Hivi karibuni Messi amekuwa akisumbuliwa na maumivu hali
inayosababisha asiwe katika hali yake ya kawaida.
0 COMMENTS:
Post a Comment