May 8, 2013




Hatimaye mshambuliaji wa Azam FC amerejea mazoezini leo na kufanya kazi na wenzake katika Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Jaffar Idd Maganga, msemaji wa Azam FC, amesema Bocco amefanya mazoezi na wenzake katika kiwango kizuri kabisa hali ambayo imewapa moyo kwamba amerejea katika hali yake.

Bocco alikuwa katika hali ngumu sana baada ya kukosa penalti wakati walipoivaa FAR Rabat ya Morocco mjini Rabat na kumalizika kwa kufungwa kwa mabao 2-1.


Iwapo Bocco angefunga na matokeo kuwa 2-2, basi Azam FC ingekuwa imesonga mbele katika nafasi ya bao la ugenini.

Baada ya kukosa penalti hiyo Bocco alikuwa katika hali mbaya na muda mwingine alikuwa akilia na kugoma kula chakula.

“Leo amerudi mazoezini, uongozi na wadau wengine wa Azam FC walilazimika kukaa naye na kumueleza kuhusiana na kilichotokea. Ndiyo soka na maisha yanaendelea,” alisema Maganga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic