Mshambuliaji nyota wa QPR iliyoteremka daraja kutoka Ligi Kuu England msimu huu, Loic Remy anashikiliwa na Jeshi la Polisi la London akituhumiwa kumbaka mwanamke kwa kushirikiana na wenzake.
Tayari Remy amehojiwa na jeshi la polisi limesema limeanza uchunguzi kuhusiana na suala hilo, ITV News ya England imeripoti.
Remy, 26, anatuhumiwa kumbaka mwnaamke huyo mwenye umri wa miaka kati ya 30-35 ambaye alimtembelea nyumbani kwake na kumkutana na binamu zake.
Mwanamke huyo amelieleza jeshi la polisi kwamba, baada ya kufika Remy alimpatia kinywaji kama mgeni, naye alimuamini na kunywa.
Baada ya muda alianza kujisikia vibaya na baadaye akalala, baada ya fahamu kumrudia alijikuta akiwa uchi na baadaye akagundua kuwa aliingiwa.
Polisi wamesema: “Maofisa katika kituo cha Sapphire wanaendelea kuchunguza suala hilo, maana mwanamke huyo amesema baada ya kushituka aliwakuta Remy na ndugu zake wakiendelea na shughuli zao kama kawaida lakini akagundua alikwua amebakwa na tukio hilo limetokea Mei 6 katika eneo la West London.:”
Wengine waliokuwa na Remy siku hiyo wnaakadiriwa kuwa na umri 22 na 23 na tayari wameishakamatwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment