Milovan akiwa na Barthez wakati akiwa Simba.... |
Na Saleh
Ally
KOCHA wa
zamani wa Simba, Milovan Cirkovic, ameamua kufungua mdomo wake kwa mara ya
kwanza na kuizungumzia mechi ya watani, Yanga na Simba inayotarajiwa kuchezwa
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Milovan,
raia wa Serbia, amesema huenda Yanga wakawa wanajidanganya kwa kuamini Simba ni
rahisi kwa kuwa inatumia wachezaji vijana, kitu ambacho si sahihi.
Akizungumza
kutoka Cacak, Serbia, Milovan alisema mechi hiyo itakuwa ngumu na si kama namna
watu wanavyoichukulia kirahisi.
“Bado Simba
wana timu nzuri ya kushindana, wanaweza kupambana na kufanya vizuri, sidhani
kama itakuwa kama wanavyoamini mashabiki.
“Vijana
walio Simba uwezo wao ni mzuri na wanaweza kupambana na kufanya vizuri. Si
sahihi kuwachukulia kwamba watapoteza.
“Lakini pia
Simba ili wafanye vizuri, hawapaswi kuwa waoga, badala yake wanatakiwa
kupambana kama wanaume. Soka ni mchezo wa wanaume,” alisema Milovan.
Milovan
ndiye kocha aliyeiongoza Simba kuweka rekodi nyingine kwa kuichapa Yanga kwa
mabao 5-0 katika mechi ya mwisho ya kufunga msimu uliopita huku ikiwa tayari
imeshabeba ubingwa.
Katika
mechi ya watani hao mzunguko wa kwanza, matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1, Yanga
wakisawazisha kupitia Said Bahanuzi kwa mkwaju wa penalti baada ya bao la
mapema la Amri Kiemba.
Mechi hiyo
ya bao 1-1 ilikuwa ya Milovan ambaye alifutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa
na Mfaransa, Patrick Liewig, atakayekuwa anapambana katika benchi Jumamosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment