Chelsea imefanikiwa kutwaa Kombe la Europa League baada ya kuichapa
Benfica ya Ureno kwa mabao 2-1.
Katika mechi hiyo ya fainali iliyopigwa mjini Amsterdam nchini Uholanzi,
Chelsea walipata mabao yao kupitia kwa Fernando Torres na Branislav Inavovic na
Benfica wakapata hilo moja kupitia Cardozo.
Torres aliichambua ngome ya Benfica hadi kipa kabla ya kupachika bao na
Cardozo akafunga kwa mkwaju wa penalty baada ya Azpilicueta
kunawa mpira ndani ya 18.
Lakini ikionekana kama mechi ndiyo imemalizika,
Ivanovic alifunga kwa kichwa baada ya kona kuchongwa wakati mwamuzi wa akipa
akiwa ameinua ubao kuonyesha dakika 90 zimekamilika.
Baada ya bao hilo, machozi ya mashabiki na wachezaji
wa Benfica yalitawala uwanjani hapo, kwani karibu kila mmoja alishindwa
kujizuia na kububujikwa na machozi.
Kocha Rafa Benitez ambaye alikuwa hatakiwi na
mashabiki wa Chelsea naye alikuwa na furaha kubwa baada ya ushindi huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment