Pamoja na kubariwa na maumivu mwili mzima, beki kisiki wa Real Madrid,
Sergio Ramos huenda akacheza katika mechi ya fainali ya Copa del Rey dhidi ya
Atletico Madri, kesho Ijumaa.
Ingawa Madrid wamefanya jambo hilo siri kubwa, lakini kuna taarifa
watalazimika kumtumia Ramos kutokana na ushawishi wake uwanjani.
Kumekuwa kuna juhudi za makusudi ili kuhakikisha mwili wa Ramos unarudi
katika hali nzuri ingawa inaonekana hatakuwa fiti kwa asilimia mia.
Ramos amekosa mechi nyingine za Madrid ilipokutana na Valladolid, Málaga
na Espanyol. Lakini amekuwa chini ya uangalizi ili acheze mechi hiyo.
Kitu kingine kinachofanya Madrid ilazimike
kuhakikisha Ramos anacheza ni kukosekana kwa Raphael Varane raia wa Ufaransa aliyefanyiwa
upasuaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment