May 14, 2013




Mshambuliaji wa Galatasaray amewatolea uvivu mashabiki wa Fenerbahce waliomuita nyani.

Mashabiki wa Fenerbahce walimuonyesha ndizi huku wakimuita nyani wakati timu hiyo iliposhinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Galatasaray.

Katika mechi hiyo Jumapili, Galatasaray tayari walikuwa mabingwa lakini walihitaji ushindi kushangilia kombe lao.

Mcameroon Pierre Webo alifunga mabao yote mawili ya ushindi ya Fenerbahce.

Drogba aliandika katika ukuta wake wa Facebook akisema mashabiki hao waliona wivu kutokana na Galatasaray kuwa bingwa.

Lakini aliwashangaa kumuita yeye nyani wakati aliyefunga mabao yote na kuwafanya wao washerekee pia atakuwa ni ‘nyani’.

“Nashangazwa, kama mimi ni nyani, aliyefunga na kusababisha mshangilie naye ni ‘nyani’.

“Vipi mtu anajiita ni shabiki sahihi wakati anayewapa furaha mnamuita nyani,” alieleza katika ukuta wake huo wa Facebook akionyesha kukerwa na kubaguliwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic