May 14, 2013


Kazi (kulia) akiwa na waamuzi wenzake..


Mwamuzi maarufu jijini Dar es Salaam, Othman Kazi amenusurika kifo katika ajali mbaya ya bodaboda jijini Dar es Salaam.

Kazi amenusurika kifo baada ya kugongwa leo asubuhi katika eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam wakati akivuka barabara.
Bodaboda hiyo ilimgonga na kumuumiza kazi vibaya ikiwa na pamoja na kusababisha kuteguka kwa bega lake moja.

Akizungumza leo akiwa nyumbani kwake, Kazi alisema anaendelea vizuri lakini anasikia maumivu makali.

“Kweli nimeumia, jamaa alikatiza pembeni ambako tunapita waenda kwa miguu na kunigonga.
“Ajali ilikuwa mbaya sana kwangu lakini  namshukuru Mungu naendelea vizuri hadi sasa,” alisema Kazi.

Refa huyo aliwahi kuwa mmoja wa waamuzi mahiri we Ligi Kuu Bara nchini kabla ya baadaye kuamua kufanya kazi zake za uamuzi katika matamasha mbalimbali kupitia kampuni yake binafsi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic