May 8, 2013




Saleh Ally
Neema tena kwa beki Shomari Kapombe wa Simba ambaye amekuwa wa kwanza kupata nafasi ya kufanya majaribio na klabu ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu England.

Wako wengine wanaoweza kupata nafasi hiyo, inategemea na uamuzi wa klabu ya Simba, mfano Mrisho Ngassa, kama atakuwa ameongeza mkataba na klabu hiyo inayotumia rangi nyekundu na nyeupe.

Huku kukiwa na taarifa kwamba anatakiwa kwenda kufanya majaribio nchini Uholanzi, Kapombe amepata bahati hiyo baada ya ujumbe wa Simba ulioungwa na Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage na Mlezi, Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa nyuki kufanya mazungumzo na mmiliki wa Sunderland, Ellis Short.

Akizungumza jana mchana kutoka Newcastle, England, Malkia wa nyuki alisema wamekubaliana mambo kadhaa na Short ambaye ni mmoja wa mamilionea nchini England, lakini suala la kina Kapombe kufanya majaribio ni kati ya mambo yaliyopita.


“Kama nilivyoeleza awali, kumekuwa na mambo mengi tumejadili lakini suala hilo la wachezaji wa Simba kuja hapa kufanya majaribio tumelipa nafasi kubwa pia.

“Tunajua tuna vijana wengi ambao wana uwezo mkubwa, mfano tulipoenda kuangalia mechi ya vijana kati ya Sunderland na Newcastle, nilimueleza Short kwamba wachezaji vijana wa Simba wana uwezo mkubwa ukilinganisha na wake, akacheka sana.

“Labda aliona kama namtania, lakini nikamuambia tuwaleke huku kwa ajili ya majaribio. Najua wakija huku watawaweka kwenye timu za vijana hasa kama watafuzu.

“Halafu taratibu wataanza kuwapandisha taratibu, waliniambia kupanda kunategemea na mcehzaji mwenye. Inaweza kuwa haraka au taratibu,” alisema Malkia wa nyuki.

Alipoulizwa kuhusiana na suala la kwenda kufanya majaribio itakuwa ni siku gani, alisema:

“Hapa inategemea tutakavyojipanga pamoja na mipango yao wao, maana yake litakuwa ni suala la mawasiliano na baada ya hapo wachezaji watakuja huku. 

“Furaha kwangu ni kwamba wamekubali na aliyepitisha hilo ni mmiliki wa klabu mwenyewe.”

Malkia amezungumzia mambo mengi kuhusiana na mkutano wao na mmiliki huyo wa Sunderland. Zaidi soka ukurasa wa 23.

SOURCE: GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic