Washambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu wataikosa mechi ya kirafiki ya Taifa Stars dhidi ya Sudan
mjini Addis Ababa, Juni 2.
Stars inatarajia kuondoka nchini Mei 26 kwenda Ethiopia
kwa jili ya mechi ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco kwa ajili ya mechi hiyo
ya mashindano.
Wachezaji hao watakuwa na kibarua siku hiyo wakati
TP Mazembe itakapokuwa inapamabana na Liga M mjini Maputo, Msumbiji katika
mechi ya Kombe la Shirikisho.
Katika mechi ya kwanza, TP Mazembe ikiwa nyumbani
iliikung’uta Liga M kwa mabao 4-0, Samatta akifunga moja.
Hivyo inaonekana haitakuwa mechi ngumu kwao, lakini
TP Mazembe imeamua wajiunge na Stars moja kwa moja ikiwa Morocco Juni 4.
Stars itakuwa tayari imetua Morocco tayari ikifanya
maandalizi ya mwisho ya mechi dhidi ya wenyeji Juni 8, mechi ya kuwania kucheza
Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Katika mechi ya kwanza jijini Dar, Stars iliwapa
Waarabu hao mzigo wa mabao 3-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment