Kocha wa
timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amewatosa wakongwe Ronaldinhona Kaká
katika kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Confederations Cup inayoanza
Juni, mwaka huu.
Michuano
hiyo huwa ni sehemu ya Kombe la Dunia, pamoja na kuwatosa wakongwe hao, Scolari
amewaita Neymar, Lucas Moura, Fred na Oscar kama wachezaji nyota zaidi.
Kati ya
watu walioitwa na kuwashangaza wengi ni kiungo Jadson wa São Paulo na Bernard
anayetarajiwa kujiunga na Atlético Mineiro.
Pamoja na Neymar,
Fred na Oscar, kocha huyo amemchukua mshambuliaji mwenye mabavu Hulk
anayekipiga FC Zenit Saint Petersburg.
Kocha huyo
anajulikana kwa kuwa na misimamo mikali muda wote na amekuwa hajali kelele za
watu hata kidogo.
Wengine ambao
amewaacha katika kikosi chake wakati walitegemea kuitwa ni mshambuliaji wa Corinthians,
Alexandre Pato, pia kiungo wa Chelsea, Ramires.
Wengine aliowatosa ni beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo na beki wa kulia wa
Barcelona, Daniel Alves.
Brazil itacheza na Japan katika ufunguzi wa Confederations
Cup, mechi hiyo itachezwa Juni 15 mjini Brasilia. Baada ya hapo, siku nne
baadaye Brazil itacheza na Mexico ambao
ni wapinzani wao wakubwa.
Kikosi kamili
cha wachezaji 23 alichoteua Scolari, hiki hapa;
0 COMMENTS:
Post a Comment