May 14, 2013



 
SAANYA (KATIKATI) AKIWA NA WAAMUZI WENZAKE

Refa huyo aliwahi kuwa mmoja wa waamuzi mahiri we Ligi Kuu Bara nchini kabla ya baadaye kuamua kufanya kazi zake za uamuzi katika matamasha mbalimbali kupitia kampuni yake binafsi.

Saa chache baada ya kuteuliwa kuchukua nafasi ya Israel Nkongo Mujuni, mwamuzi Martin Saanya atakayechezesha pambano la Yanga na Simba Jumamosi amekuwa gumzo.

Mwamuzi huyo kutoka Morogoro amekuwa gumzo baada ya kupewa nafasi hiyo na Salehjembe imegundua kuwa ni shabiki mkubwa wa Real Madrid.


Mwamuzi huyo amekuwa akivaa ‘kifuta jasho’ mkononi chenye nembo ya klabu hiyo ya Hispania karibu kila mechi anayochezesha.

Mechi kadhaa zimeonyesha Saanya akiwa amevaa ‘kifuta jasho’ hicho katika mkono wake wa kushoto kuonyesha yeye ni shabiki mkubwa wa Madrid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic