May 9, 2013



Wakati Manchester United wakiwa wametangaza kwa asilimia 95 kuwa kocha wao mpya ni David Moyes, rekodi yake ya ugenini imeonekana kuzua mjadala.

Katika mechi 45 alizoiongoza everton dhidi ya timu kubwa za Man United, Chelsea, Liverpool na Arsenal, hakuwahi kushinda hata mechi moja ya ugenini.

Katika mechi hizo, Moyes alishindwa mechi 27 na sare 18 huku akiwa amepoteza 27 hivyo kuanzisha hofu kwamba kama ataweza kuingoza United kushinda mechi zake za ugenini.

Kwa kiasi kikubwa kunaonekana kuwa na hofu kuhusiana na mambo yanavyokwenda na kama kocha huyo atauweza muziki wa Man United.
Hofu nyingine ni kuhusiana na michuano ya kimataifa barani Ulaya na inaonekana hana uzoefu, kitu ambacho kitafanya alazimike kujifunza akiwa kazini.


REKOSI YA DAVID MOYES AKIWA EVERTON

                           P      W     D      L        Win%
Everton         516      217  139  160     42.05


Rekodi ya ugenini dhidi ya Manchester United, Chelsea, Liverpool na  Arsenal:
Cheza 45, Shinda 0, Sare 18, Poteza 27,
Pointi 18 (kati ya 135).


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic