Ratiba ya
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2013/2014 inayoshirikisha timu 24 zilizo
katika makundi matatu zikicheza kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini)
inatarajiwa kutolewa Agosti 14 mwaka huu.
African Lyon
(Dar es Salaam), Friends Rangers (Dar es Salaam), Green Warriors (Dar es
Salaam), Ndanda (Mtwara), Polisi (Dar es Salaam), Tessema (Dar es Salaam),
Transit Camp (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam) zinaunda kundi B.
Timu za
kundi C ni JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi
(Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto
Africans (Mwanza).
Tunapenda
kukumbusha kuwa dirisha la usajili kwa madaraja yote ni moja ambapo usajili wa
hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati hatua ya pili
ni Agosti 14 hadi 29 mwaka huu. Dirisha dogo litafunguliwa Novemba 15 hadi
Desemba 15 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment