Waamuzi wote
wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa utimamu wa mwili (physical
fitness test) utakaofanyika katika vituo viwili.
Mtihani huo
utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es Salaam na
Morogoro. Kituo cha Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera,
Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Kituo cha
Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani,
Ruvuma na Tanga.
Washiriki
wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si
vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki katika
mtihani huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment