Klabu ya AS Cannes ya Ufaransa imeonyesha kujivunia beki wake mpya, Shomari Kapombe kutoka Simba.
Kupitia mtandao wake AS Cannes imejivunia beki huyo ambaye alianza kujipukia kisoka mjini Morogoro mwaka 1999.
Kapombe aliyekuwa mmoja wa watoto waokota mipira sasa tayari amejiunga na AS Cannes inayoshiriki daraja la nne nchini Ufaransa.
Klabu hiyo
imeonyesha wazi kuvutiwa na ambaye pamoja na kuwa na miaka 21 lakini amekuwa
tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa.
Mtandao huo
umeelezea kuhusiana na namna kocha wa timu hiyo, Jean-Marc Pilorget anavyoweza
kutatua matatizo yake kadhaa kwa kumtumia Kapombe.
Kapombe
ameunganishwa na AS Cannes kupitia wakala wake, Denis Kadito ambaye anaishi
Uholanzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment