SIKU TAMBWE ALIPOTUA SIMBA... |
Kibadeni
maarufu kama Mputa, amesema kasi ya mshambuliaji huyo raia wa Burundi imemshtua
na kumfurahisha.
“Ilikuwa ni
siku ya kwanza, achana na kwamba alifunga bao, lakini kasi yake uwanjani
ilikuwa nzuri sana.
“Sikutegemea
yeye na mwenzake (Demunga) wangecheza hivyo. Maana walisafiri kutoka Dar es
Salaam hadi Shinyanga, walipanda ndege na baadaye gari.
“Walifika
hapa Shinyanga saa nane mchana na wakakubali kucheza. Wote wawili walicheza
vizuri na uwezo ulikuwa mkubwa,” alisema Kibadeni.
Kocha huyo
amesema anatarajia makubwa kutoka kwa wachezaji hao lakini zaidi ni kuwapa
ushirikiano na wao kujituma.
Katika mechi
hiyo ya kirafiki dhidi ya Shinyanga Stendi, Simba ilishinda hilo bao 1-0 likiwa
limefungwa na Mrundi huyo.
Simba
inatarajia kuanza Ligi Kuu Bara keshokutwa dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora ambayo
ndiyo imepanda daraja msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment