Na Khatimu Naheka, Arusha
Katika hali ya kushangaza, kiungo wa
JKT Oljoro, Udda Sorita alijisaidia haja ndogo uwanjani huku sababu kubwa
ikatajwa kuwa uchafu wa vyoo vya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili
cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya timu yake dhidi ya Simba, juzi kwenye ambapo
Simba ilishinda bao 1-0.
Mchezaji huyo alifanya tukio hilo
wakati alipokuwa akipasha misuli huku mechi ikiendelea, ambapo aliketi chini na
kujisaidia na alipomaliza alikwenda kwa mwamuzi wa akiba na kuingia uwanjani akichukua
nafasi ya Essau Sanu.
Alipouliza juu ya tukio hilo, kiongozi
wa JKT Oljoro ambaye hakutaja jina lake litajwe alisema: “Kama kafanya hivyo
mimi simlaumu kabisa kutokana na hali ya uchafu iliyopo kwenye vyoo vya uwanja
huu, kawaambie viongozi wa uwanja wafanye usafi vyooni.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment