KITENGE, ALIYEFIWA NA BABA YAKE MZAZI.... |
Mchezaji wa zamani wa Yanga
na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74) ambaye ni baba wa mtangazaji maarufu wa
michezo, Maulid Kitenge amefariki dunia.
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza
kupokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa
Stars, Baraka Kitenge (74) kilichotokea leo mchana (Agosti 20 mwaka huu) jijini
Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani
kwa nyakati tofauti Kitenge akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu
mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Kitenge amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
ambapo alikuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake
katika Yanga na Taifa Stas alicheza na wachezaji kama akina Athuman Kilambo na
Abdulrahman Juma.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu,
Yombo Vituka (Jet) jijini Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge
mahali pema peponi. Amina
0 COMMENTS:
Post a Comment