Wachezaji wawili wa kigeni wa Azam FC,
Humphrey Mieno na Brian Umony watarajiwa kurejea uwanjani hivi karibu baada ya
hali za afya zao kuimarika na kuanza mazoezi kwa ajili ya kuungana na wenzao
kwenye mechi za Ligi Kuu Bara zilizoanza kwa msimu wa 2013/2014.
Akizungumza na Championi Ijumaa juu ya wachezaji hao waliokuwa majeruhi kw amuda
mrefu daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa alisema:
“Mieno na Umony wanaendelea vizuri kwa
sasa hali zinaridhisha kwa kweli na natumai mechi zijazo wanaweza kurejea
uwanjani.
“Pia kwa upande wa beki Haji Nuhu
anaendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi lakini hatawezi kucheza siku hizi za
karibuni yeye yuko kwenye matibabu ya goti lake.”
Mieno alipata matatizo kwenye nyama za
paja na Umony alipata matatizo katika mguu wake na kufungwa P.O.P.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment