Kocha wa
zamani wa Simba, Milovan Cirkovic amesema atarejea kwao Serbia na kuachana na
kazi.
Milovan
ambaye sasa yuko nchini Kuwait akiinoa timu ya Al Sad upande wa kikosi cha
vijana.
Akizungumza
kutoka Kuwait City, Milovan alisema ofa aliyopewa anaona ni ndogo.
“Najaribu
kuzungumza nao kama watakubaliana nami basi waongeze.
“Lakini
ishindikana nitarejea Serbia kuwa siwezi kufanya kazi katika kiwango cha fedha
wanachotoa,” alisema.
Timu yake ya
mwisho ilikuwa Simba ambayo pia ilikatiza mkataba wake na kuchelewesha malipo
yake hadi alipojitokeza Malkia wa Nyuki na kumlipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment