TAMBWE WA KWANZA KUSHOTO WALIOSIMAMA NA DEMUNGA WA KWANZA KULIA WALIOSHIKA MAGOTI WAKIWA NA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA BURUNDI KILICHOFUZU MICHUANO YA CHAN. |
Uongozi wa Simba umelia kufanyiwa faulo kuhusiana na wachezaji wawili Gilbert Kaze 'Demunga' na Amis Tambwe.
Lakini Salehjembe imeibua njama za klabu ya Vital'O na Chama cha Soka cha Burundi kutaka kuwazuia wachezaji hao wasicheze Simba.
Pamoja na wachezaji hao kuwa wamemaliza mkataba na Vital'O, klabu hiyo iliwazuia na kudai inataka kulipwa, Simba ikaona haina ujanja, ikatoa dola 10,000 ili waachiwe.
Lakini Vital'O kwa kushirikiana na viongozi wa shirikisho lao wameendelea kuibania Simba kutoa kibali.
Ukweli ni kwamba wanafanya hivyo kwa kuwa iwapo wataanza kuichezea Simba, watakuwa wamepoteza haki ya kushiriki Michuano ya Chan.
Wakati wa kufuzu michuano hiyo, Demunga na Amis ndiyo walikuwa chachu ya kuing'oa Sudan.
Hali hiyo ndiyo inafanya wao waendelee kuwabania ili wasicheze Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment