Mchezaji kiraka, Kabange Twite
amefunguka wazi kuwa hataki kuichezea Yanga, badala yake anajipanga kuelekea
Qatar kucheza soka la kulipwa kama ilivyo kwa Mwinyi Kazimoyo ambaye yupo huko
akiichezea Klabu ya Al Markhiya.
Kabange ambaye yupo jijini Dar es
Salaam kwa muda wa wiki kadhaa sasa, alikuwa aichezee Yanga lakini
ikashindikana kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya mipango ya usajili. Ameliambia
gazeti hili kuwa hana mpango huo wa kuichezea Yanga lakini akashindwa kutaja
sababu za kuchukua uamuzi huo.
“Mimi ninapita tu hapa Tanzania
naelekea Qatar kufanya majaribio ya kucheza soka, sasa hivi namngoja meneja
wangu, amerudi Congo kuchukua fedha ndiyo tuendelee na safari yetu.
“Yanga naipenda sana kwani ni timu
nzuri, watu wanapendana na wanaonyeshana ushirikiano wa hali ya juu, hivyo
watapata mafanikio makubwa hata bila mimi kuwepo,” alisema Kabange.
Akizungumzia juu ya uamuzi wa ndugu
yake, Mbuyu alisema hatapenda Kabange arejee kwa sasa Yanga bila kufafanua kwa
undani.
0 COMMENTS:
Post a Comment