September 6, 2013



 
VIGOGO WA TASWA, JUMA PINTO (KATIKATI), AMIR MHANDO NA MAULID KITENGE , NYUMA NI GEORGE JOHN
Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo, Taswa FC, imefanikiwa kupata msaada wa Sh milioni 5.2 kutoka kwa wadau mbalimbali wa michezo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, jana, Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto alisema kiasi hicho cha fedha ni maalum kwa kufanikisha safari ya timu hiyo katika kushiriki bonanza la habari litakalotimua vumbi keshokutwa jijini Arusha.

Pinto amesema tayari uongozi wake umepokea kiasi hicho cha fedha ambapo katika fungu hilo, Sh milioni moja imetolewa na mfanyabiashara Kassim Dewji, Chama cha Soka jijini Dar (DRFA) kimetoa Sh milioni 1.2, Davis Mosha akamwaga Sh milioni 3.

Kampuni ya Azam nayo imetoa mchango wake ambao haikutaka kuuweka wazi. “Fedha hizo zote tumeshazipata na timu zote kuanzia ile ya wanaume na hata ile ya wanawake ya netiboli, nayo ipo sawa kabla ya safari hiyo, tunatarajia kuondoka Jumamosi (kesho), tunawashukuru wadau wote waliotuchangia katika safari yetu,” alisema Pinto.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic