Mshambuliaji
wa zamani wa Simba, Khalfan Ngassa amempoteza mama yake mzazi ambaye amefariki
dunia jana.
Mama mzazi wa
Khalfan ambaye ni bibi wa mshambuliaji nyota wa Yanga amefariki jijini Mwanza,
jana.
NGASSA AKIWA NA BIBI NA BABU YAKE |
Akizungumza,
Ngassa alisema bibi yake huyo amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
“Baba
kanitaarifu muda mfupi uliopita, sijajua kuhusiana na mazishi yatakuwa lini
hadi hapo nitakapowasiliana naye tena,” alisema Ngassa ambaye sasa hachezi
akitumikia adhabu ya kusimamishwa mechi sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment