November 25, 2013




Mwenyekiti wa Simba, aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage amewarudisha kazini makocha Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’.
 
Rage ametangaza leo kwamba Kibadeni na Julio wataendelea na kazi yao na si kocha Logarusic.

Baada ya rage kusimamishwa na kamati ya utendaji ilitangaza kuwaondoa makocha hao na nafasi yao kuchukuliwa na Logarusic raia wa Croatia lakini Rage na akawapinga na kujirudisha madarakani.

Mgogoro ndani ya Simba unazidi kuwa mkubwa kwani Rage amekuwa na upande wake huku kamati ya utendaji nayo ikisimamia upande wake.

“Kweli nimewarudisha Kibadeni na Julio na hawa ndiyo makocha wa Simba na wataendelea na kazi,” alisema Rage leo hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic