November 25, 2013



 
MWOMBEKI AKINYOOSHWA MISULI NA DAKTARI WA SIMBA
Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki, ameonyesha kuwazidi nyota wenzake wa kikosi hicho kwa kuendelea kujifua katika mazoezi yake binafsi ambayo yamemghalimu kulipa kiasi fulani cha fedha.


 Mwombeki amesema katika mazoezi yake hayo anayoyafanya jijini Mwanza, amekuwa akimlipa Sh 50,000 kwa wiki kocha maalum anayemnoa, Athuman Bilal.

Mwombeki amesema tayari ameshajifua kwa wiki tatu sasa ambapo mazoezi hayo yataendelea mpaka kukaribia kwa ufunguzi wa kambi ya kikosi hicho, ambacho kinatarajiwa kuanza rasmi maandalizi Desemba Mosi kikiwa na kocha mpya, Mcroatia, Zdravok Logarusic.
“Nimepanga kujiweka sawa, unajua huku nipo na kocha wangu Bilal (Athuman) na nimekuwa nikimlipa shilingi elfu hamsini kwa wiki, nataka kuwa tayari kabla ya kuja kwenye mazoezi ya timu nzima,” alisema Mwombeki.

 “Mpaka sasa nimeshakuwa kwenye mazoezi haya kwa wiki tatu sasa, nitaendelea hivi mpaka kukaribia kwa kambi ya timu nzima, wakati naanza nilikuwa nafanya kwa siku mara mbili lakini wiki hii (iliyopita) nimeanza kufanya mara moja kwa siku.”

Mwombeki ameumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao manne. 
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic