November 25, 2013



 
CHOLLO WA KWANZA KUSHOTO WALIOSHIKA MAGOTI, AKIWA NA KIKOSI CHA SIMBA
Nahodha wa pembeni na nahodha wa Simba, Said Nassor ‘Chollo’, amewashauri viongozi wa klabu hiyo wahakikishe wanamnasa kipa Ivo Mapunda anayeichezea Gor Mahia ya Kenya.


Simba inadaiwa kumhitaji kipa huyo katika usajili huu unaoendelea kwenye Ligi Kuu Bara.

Ivo anatarajiwa kumaliza mkataba wake na Gor Mahia mwezi ujao na Simba inahitaji kipa kutokana na Abel Dhaira kushindwa kukata kiu ya mashabiki katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Chollo alisema kutokana na kiwango alichonacho Ivo ukichanganya na uzoefu alionao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, litakuwa ni jambo jema kama akitua Msimbazi.

“Bado ni golikipa mzuri kwa uwezo wake niliouona kwenye mechi ya Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe, halafu ukizingatia ameipa ubingwa Gor Mahia, kwa hiyo ni mtu anayefaa, itakuwa ni vizuri kama akija tusaidiane kuipeleka Simba mbali zaidi,” alisema Chollo.

Simba imemaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya nne ikiwa imefungwa mabao 13 ambayo yanaleta wastani wa kuruhusu bao moja kwenye kila mchezo

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic