November 25, 2013



 
VIALLI
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Salum Bausi, amemteua kiungo wa Azam FC, Hamis Mcha kuwa nahodha wa kikosi hicho katika michuano ya Chalenji.


Michuano ya Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa jijini Nairobi, Kenya.

Mcha ameteuliwa kushika wadhifa huo badala ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ametemwa katika kikosi hicho.

 Bausi amesema ameamua kumpa kitambaa hicho Mcha kutokana na nidhamu kubwa ambayo amekuwa akiionyesha tangu akiwa na klabu yake mpaka kwenye timu ya taifa.

“Ni kijana mwenye nidhamu ya hali juu, iwe kwenye klabu yake ama hapa. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengine. Nina imani naye kuweza kuongoza kundi la watu wazima kutokana na nidhamu anayoionyesha kila siku,” alisema Bausi.

Cannavaro na Aggrey Morris walitemwa kwa kile alichosema ni kutokana na utovu wa nidhamu wa kugawana fedha kiasi cha dola 10,000 walizopata kama tuzo ya mshindi wa tatu kwenye michuano ya mwaka jana nchini Uganda.

Bausi aliongeza kuwa, kikosi hicho kinatarajia kuondoka leo Jumatatu kwenda Kenya ili kujiweka ‘fiti’ kabla ya mchezo wa kukata utepe dhidi ya Sudan Kusini Jumatano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic