December 31, 2013







Hatimaye kipa Juma Kaseja ameanza mazoezi tena na timu yake ya Yanga.

Kaseja ameanza mazoezi baada ya kuomba ruhusa na kufanya akosekane mazoezini kwa takribani wiki moja.
Kipa huyo alishutumiwa sana na mashabiki na wanachama wa Yanga baada ya timu hiyo kuchapwa na Simba kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe.'


Hali hiyo iliyokana naye kufanya kosa lililozaa bao la tatu. Taarifa zinasema Kaseja aliomba mapumziko ili arejee vizuri kisaikolojia.

Leo asubuhi alionekana mazoezini katika Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar akijifua pamoja na makipa wenzake, All Mustapha ‘Barthez’ na Deogratius Munish ‘Dida’ wote wakiwa chini ya mwalimu wao raia wa Kenya, Razak Siwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic