IDDI PAZI AKIWA NA BLOGA, LE MUTUZ |
Simba imeingia mkataba na kocha mwingine msaidizi, Idd Pazzi ambapo sasa ni maalum
kwa kazi ya kuwanoa makipa.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Swedi Nkwabi alisema
kufuatia mazungumzo aliyoyafanya na Pazzi, maarufu kwa jina la ‘Faza’,
yaliyochukua takribani siku nne, wamekubaliana na kocha huyo na kufanikiwa
kumsainisha mkataba wa miezi sita.
“Tumekubaliana
naye na sasa ni kocha wetu akichukua nafasi ya James Kisaka, tumeingia naye
mkataba wa miezi sita na kazi ataanza mara moja leo (jana) jioni akiwa na kocha
mkuu Zdravok Logarusic na msaidizi wake, Selemani Matola,” alisema Nkwabi.
Kufuatia
kauli hiyo ya Nkwabi, Championi Ijumaa lilimsaka Pazzi katika kujua ukweli wa
taarifa hizo, ambapo alikiri kumalizana na Simba huku akisema maamuzi hayo
hayakuwa rahisi kutokana na timu yake ya zamani ya Ashanti kuonyesha bado
ilikuwa ikimhitaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment