Kipa wa zamani wa Simba, Andrew Ntalla anatarajia kwenda nchini Malawi
kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu mbili tofauti.
Ntalla aliachwa na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo kutokana na
kuonyesha kiwango kidogo ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu alipotua klabuni
hapo akitokea Kagera Sugar.
Ntalla alisema anasubiri mwaka mpya upite ndipo aende kufanya majaribio katika timu hizo ambazo alidai ni mapema kuzitaja kwa kuwa mambo bado hayajakamilika vizuri.
“Nashukuru nimeshamalizana na Simba, mchakato wa kunitafutia timu
umefanywa na meneja wangu raia wa Malawi ambaye alikuwa akinifahamu tangu nipo
Kyela, Mbeya,” alisema Ntalla.
0 COMMENTS:
Post a Comment