Kocha Mkuu
mpya wa Azam FC, Joseph Omog, ameondoka nchini kuelekea kwao Cameroon mara
baada ya kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Taarifa
kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, kocha huyo ameondoka kwenda
kupumzika na atarejea baada ya wiki mbili kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
“Kocha ameondoka
Jumatano (juzi) kuelekea nchini kwake kwa ajili ya mapumziko ya wiki mbili
kisha atarejea tena hapa nchini ili kuanza kukinoa kikosi chetu.
“Baada ya
kurejea, ataendelea na majukumu yake kama kawaida na kuweka mikakati na mipango
madhubuti kwa ajili ya timu yake na hata kuweza kufahamu anajipanga vipi katika
kuhakikisha anaifikisha timu mbali,” alisema mtoa taarifa wetu.
Alipoulizwa
juu ya hilo, Katibu wa Azam FC, Idrissa Nassoro, alisema: “Kocha ataondoka
kesho (leo Ijumaa) na timu itakuwa chini ya Kali Ongala.”
0 COMMENTS:
Post a Comment