Koccha Msaidizi
wa Yanga bana kwa utani! Felix Minziro, juzi kaaga kuwa atasafiri kuelekea Malaysia
kwa ajili ya kumsindikiza mshambuliaji wake Said Bahanuzi kwenda kufanya
majaribio ya kucheza soka la kulipwa, lakini kumbe amekwenda Zanzibar.
Minziro,
juzi aliwaambia waandishi wa gazeti hili kuwa alikuwa mbioni kusafiri kwenda
nchini humo na atakaporejea ndiyo atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia
Yanga lakini kumbe mmm!
“Sijasaini
mkataba mpya Yanga ila natarajia kusaini baada ya kurejea kutoka huko (Malaysia)
kwani natarajia kumsindikiza Bahanuzi na nitamuacha huko kisha mimi nitarudi,”
alisema Minziro juzi.
Lakini jana blogu hii ikapata taarifa kuwa, Minziro hakusafiti na
Bahanuzi ambaye aliondoka jana Alhamisi, bali alikuwa ni miongoni mwa makocha
20 walioteuliwa na rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
kuhudhuria semina fupi ya siku tatu visiwani Zanzibar ambapo yuko huko.
0 COMMENTS:
Post a Comment